Wednesday, December 21, 2011

Gharika la leo Jangwani

Barabara ilifungwa kuanzia mwanzo wa daraja ukitokea fire

Maji yalisambaratisha watu walokua magomeni walibaki huko huko na wa fire walibaki pande hiyo hiyo



Sehemu ya yard ya magari lifurika pia

Askari walokua wakifanya kazi ya kuokoa watu walokua wamenasa kwenye miti wakipita kwenda kufata vifaa vingine vya uokoaji

Askari badala ya kujitahidi kuokoa watu majini walizidisha nguvu kufukuza watu walokua na hofu na ndugu zao walokua majini

Mbioo watu wakitimuliwa na askari


Watu wakawekwa hapo na hiyo kamba ikapitishwa hamna mtu kuvuka
Chezea wabongo,walivuka hivyo hivyo wakarudi kule kule walipokua karibu na maji yalipofurika

Haoooo wakirudi zao

Mwanzo Sikuelewa hizi mbao zina kazi gani nkabaki nmeduwaa tu 

Jangwani hiyo..





Hivi vitu vilikua vinapelekwa na maji aliyejiokolea ndo alikua anaweka pembeni



Zle mbao ndo zilitengeneza kitu hichi cha kuvusha watu hapo jagwani

Hilo tope sasa..





FFU wakaanza kufukuza watu na hapo ndo ikawa time yangu na mie ya kujisepesha kwa sababu za kiusalama zaidi
Nkaishia zangu...