Hili gari lilipata mtafaruku katika eneo la mbwewe barabara ya Chalinze-segera
Nilishuka nikaenda kupata picha ya karibu ya hilo gari
Hao ni abiria walokua wamejichokea vya kutosha huku wasijue hatma ya safari yao,ukicheki nauli 18,000 halafu wengine hata hawawezi ku afford nauli ya basi jingine halafu na watoto ndo kama hivyo,lazma ukasirike..
Mbele kidogo eneo la komkonga basi jingine likawa katika kasheshe
Inavyosemekana basi hili lilipata ajali ya moto wiki iliyopita na wiki hii ndo hivyo likawa limedondoka,watu waliokua eneo hilo walionekana kutotaka kupigwa picha na kama uonavyo hadi jina labasi likatiwa tope lisisomeke
Tartiibu nikaondoka eneo la tukio kabla sijavamiwa nikapata manundu ya uso..
Hapo nilikua safarini jana and soon nitawaletea yaliyojiri katika hiyo safari yangu