Hey guys sorry nilikua kimya this week nlipata kisafari cha ghafla ila njiani nilikutana na tukio kama hili
Hili ni gari lilokua limebeba shehena ya mahindi likiteketea kwa moto katika eneo la ruvu darajani kama uonavyo hapo juu,full mijihasara,inauma,dduh!
Nilijaribu kuuliza kwa waliokua eneo la tukio nikaambiwa dereva wa gari hilo aliambiwa kuwa gari lake lilikua na tatizo taingia usiku wa saa tisa ila hakutilia maanani hadi hapo lilipomwakia moto kama hivyo,ilikua mida ya saa mbili asubuhi wakati nikipiga picha hizi
Gari lionekanavyo kwa mbele
Watu wakisevia mahindi kiulaiiiiiiniiii,ama kweli kifo cha panzi sherehe kwa kunguru
Popcorn hizo zilizookotwa tayari kwenda kukoboewa watu wakajisevie